wahamiaji zaidi ya 2000 waokolewa


Wahamiaji wakiwa kwenye boti ndogo kabla ya kuokolewa.
Walinzi wa pwani ya Italia wameongoza shughuli ya kuwaokoa wahamiaji 2,000 ambao walituma ishara ya kuwa taabani kwenye mashua nje ya pwani ya Libya.
Baadhi ya wahamiaji waliookolewa.
Bahari baina ya Libya na Italia, ndio njia inayotumiwa kwa muda mrefu na wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ili kuingia Ulaya.Umoja wa Mataifa umesema kuwa bahari ya Mediterranian ndio kivukio maarufu.Kufikia sasa takribani watu laki moja wamewasili katika ufukwe wa Italia, wengine zaidi ya laki moja na nusu waliwasili Ugiriki.
Meli ya Norway ikishiriki oparesheni hiyo.
Jarida moja la Norway, Aftenposten limesema kuwa manuari ya kijeshi ya taifa hilo, Siem Pilot liko njiani kuwasaidia wahamiaji hao walioko mashakani, Manuari hiyo iliwaokoa wahamiaji 320 mapema leo kabla ya kurejeshwa tena kushiriki operesheni hiyo ya kuokoa nafsi za watu wanaokisiwa kuwa takriban 3,000.

0 Comment "wahamiaji zaidi ya 2000 waokolewa"

Post a Comment

Thank you for your comments