Jokate Mwegelo hatoki begani mwa mahabuba wake, Alikiba.
Wawili hao wapo jijini Nairobi, ambapo Kiba yupo kurekodi kipindi cha Coke Studio na Jokate ameamua kuungana naye kumsaidia kumpunguzia baridi la jiji hilo ambalo kipindi hiki linadaiwa kuwa katika kilele chake.
Jokate ameshare picha kadhaa kwenye Instagram zikimuonesha akiwa na hitmaker huyo wa Mwana na pia kumshuhudia
mwandani wake huyo akirekodi wimbo anaofanya na kundi Kenya, Sauti Sol.
mwandani wake huyo akirekodi wimbo anaofanya na kundi Kenya, Sauti Sol.
Hata hivyo huenda Jokate akawa ameenda pia kufanya kazi zake binafsi kwakuwa katika picha moja anaonekana akiwa na mtangazaji mrembo wa TV wa nchini humo, Sarah Hassan.
0 Comment "Jokate Mwegelo amfwata kiba Nairobi"
Post a Comment