gauni la Kajala la mtoa kijasho Designer wake


KAJALA (3)Gauni la staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja, lilizua minon’gono ukumbini wakati wa Shindano la Kinondoni Talents Search (KTS) lililofanyika katika Ukumbi wa Millennium Tower, Makumbusho jijini Dar baada ya gauni hilo kuambatana na watu wa
kulishika.
KAJALA (4)Staa huyo aliingia ukumbini hapo akiambata na kijana mmoja akilishika gauni lake ambapo kila alipokatiza kijana huyo alikuwa na kazi ya kuzunguka naye kuhakikisha nguo hiyo inakaa vizuri bila kujikunja kitu ambacho kiliwafanya baadhi ya watu ukumbini kuanza kulishangaa gauni hilo.
KAJALA (1)Kajala alipoulizwa sababu ya gauni hilo kushikiliwa alisema: “ Wale vijana ndiyo waliolibuni gauni langu ndiyo maana walikuwa makini kuhakikisha linakuwa sawa wakati wote,” alisema Kajala.

0 Comment "gauni la Kajala la mtoa kijasho Designer wake"

Post a Comment

Thank you for your comments