Baada ya kupoteza umaarufu Rose Muhando aomba radhi

mhando2
Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili, Rose Muhando.
Brighton Masalu
MWIMBAJI nyota wa nyimbo za Injili, Rose Muhando, amewaomba radhi watu wote aliowahi kuwakwaza, ikiwa ni pamoja na kuchukua fedha za kushiriki onesho, lakini akashindwa kufanya hivyo, akidai ni ubinadamu.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Rose alikiri kuingia baadhi ya mikataba na kushindwa kuitekeleza, akisema ni jambo lililomkosesha sana raha, hasa pale watu walipokuwa wakimchukulia kama tapeli.
ROSE MUHANDO1
“Hata hivyo, mara nyingi huwa nasingiziwa, lakini nakaa kimya kwa sababu nimeumbwa hivyo, kama kuna yeyote nimemdhulumu naomba anisamehe, sikufanya makusudi, nilishindwa kutokea kwa bahati mbaya, mimi ni binadamu. Namuomba pia baba yangu mlezi Msama (Alex, Meneja wake) naye kama kuna mahali nilimkwaza kwa matamshi au matendo, naomba anisamehe,” alisema nyota huyo wa kibao cha Facebook.

0 Comment "Baada ya kupoteza umaarufu Rose Muhando aomba radhi"

Post a Comment

Thank you for your comments