Sababu za wanaume kukosa hamu ya sex



Mpenzi msomaji, leo naendelea kuelezea mambo yanayowafanya wanaume wakose hamu ya tendo la ndoa.
Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa Testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili.
Kama Thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa Thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo.
Umri kuwa mkubwa
Kiwango cha Testosterone katika mwili wa mwanaume hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadiri mwanaume anavyozidi kuwa na umri mkubwa. Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa Testosterone. Kwa mwanaume homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari.
Homoni hii ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango cha Testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanaume huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume linaweza kusababishwa na vitu vingi sana. Nikukumbushe tu kwamba sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili.
Uchovu
Wakati mwingine uchovu husababisha mtu kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Na ikiwa mtu atakuwa anasongwa na shughuli nyingi zinazochosha mwili kiendelevu hamu ya kushiriki tendo la ndoa huanza kupungua na ikizidi basi baadaye mwanaume husika atakosa hamu ya kushiriki tendo hilo na itahitaji uangalizi mkubwa ili arejee katika hali yake ya kawaida.
Vilevile kukosa mpango mzuri wa shughuli zako na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa inachangia tatizo hilo hilo. Uhusiano wa kimapenzi unataka utengewe muda wake na unaotosha.
Msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha hali inayosababisha kushindwa kuyafanya mambo yako wkiufanisi.
Usikose kufuatilia Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

0 Comment "Sababu za wanaume kukosa hamu ya sex"

Post a Comment

Thank you for your comments